Friday 31 October 2014

RAIS WA BUKINA FASO ANG'OLEWA





Rais Blaise Compaore ajiuzulu


Jenerali, Honore Traore, mkuu wa majeshi ya Burkina Faso akitangaza kuchukua madaraka ya nchi Oct 31, 2014


Mkuu wa majeshi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (kati kati),akizungumza kwenyemkutano na waandishi habari kutangaza kwamba anachukua madaraka ya nchi akiwa katika makao makuu ya jeshi mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, Oct. 31, 2014.


Waburkinabe wanasherekea tangazo la kuondoka madarakani kwa Rais Blaise Compaore baada ya kukabiliwa na upinzani mkali wa wananchi, Oct. 31, 2014.


Wapinzani wa serikali wamekusanyika kwenye Uwanja wa Taifa mjini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, ili kuhakikisha na kusherekea kuondoka madarakani kwa Compaore Oct. 31, 2014.


Watu wapora nyumba ya Francois Compaore, kaka yake mdogo rais wa zamani Blaise Compaore, mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 31, 2014.


Wapinzani wa serikali wakiimba kwa furaha mbele ya makao makuu ya jeshi mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 31, 2014.


watt wanasherekea kuondoka kea kiongozi wa muds mrefu wa Burkina Faso Rais Blaise Compaore mjini Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 31, 2014.


Mkuu wa majashi ya Burkina Faso Jenerali Honore Traore, (kati kati), akizungumza na maafisa wenzake kabla ya mkutano na waandishi habai kutangaza anachukua madaraka katika mii mkuu wa Ouagadougou, Burkina Faso, Oct. 31, 2014.


Picha ya zamani ya Rais Blaise Compaore aliyetangaza Ijuma Oktoba 31, 2014, kwamba anaacha madaraka na hivyo kufikisha kikomo miaka 27 ya utawala wake.

Mkuu wa majeshi amechukua madaraka ya kuiongoza Burkina Faso baada aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Blaise Compaore kujiuzulu.

Jenerali Honore Traore aliwaambia wana habari mjini Ouagadougou mapema leo kwamba yeye ndiye mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa sasa.

Generali huyo aliya-anza madaraka hayo jana, pale alipotangaza mipango ya serikali ya mpito na kuamrisha watu kukaa majumbani baada ya ghasia za waandamanaji kwenye makao makuu ya serikali dhidi ya Bwana Compaore.

Vyombo vya habari vya Burkina Faso vilitangaza taarifa ambayo Bwana Compaore alitangaza siku 90 za mpito kuelekea uchaguzi. Wakoloni wa zamani wa nchi hiyo Ufaransa, kwa haraka wamesema wamepokea kujuizulu kwake.

Televisheni ya “Burkina 24” imetangaza kwamba Rais huyo wa zamani aliondoka kutoka ikuli chini ya ulinzi mkubwa. Bwana Compaore ameoiongoza Burkina Faso kwa kipindi cha miaka 27 baada ya kupinduliwa na kuuliwa kiongozi mpenda mageuzi na maendeleo Thomas Sankara.

Like page yetu Facebook (Uhondo_tz)

No comments:

Post a Comment