Friday 31 October 2014

ISRAELI YACHANGANYIKIWA BAADA YA SWEEDENI KUITAMBUA PALESTINA

Israel yachanyikiwa baada ya Sweden kuitambua Palestina

Utawala haramu wa Israel umemwita nyumbani balozi wake kutoka Sweden baada ya serikali ya nchi hiyo kuitambua rasmi nchi ya Palestina.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa kuitwa balozi wa utawala huo kutoka Sweden kunaonyesha kuchukizwa Tel Aviv kutokana na hatua hiyo ya serikali ya Stockholm kuhusu Palestina. Amesema kuwa, balozi huyo nchini Sweden, Isaac Bachman, atabakia nyumbani kwa muda usiojulikana.
Hapo jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Margot Wallström alitangaza kuwa serikali ya Stockholm imeitambua rasmi nchi ya Palestina. Bi Margot alisisitiza kwamba, serikali ya Sweden inaamini kuwa, vigezo vya lazima vya sheria za kimataifa vya kuitambua rasmi Palestina kama dola ambavyo ni ardhi hata kama hakuna mipaka maalumu, watu na serikali vimetimia kwa Palestina.
Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Fauzi al-Barhum sambamba na kukaribisha hatua hiyo, amewataka viongozi wa nchi nyingine za Ulaya kuwawekea mashinikizo watawala wa Israel.

http://uhondospecialblog.blogspot.com/2014/10/31-israel-yachanyikiwa-baada-ya-sweden-kuitambua-palestina

No comments:

Post a Comment